Friday, 8 September 2017

MADHABAHU

MADHABAHU ni mahali rasmi ambapo watu au mtu hutumia kufanya ibada kwa Mungu au mungu ambaye ndiye mwabudiwa. Kuna utofauti kati ya mungu wa herufi ndongo na Mungu huyu wa herufi kubwa ya mwanzo , huyu ni mungu wa dunia hii ambaye hakuumba mbingu na nchi ,ila Mungu wa herufi kubwa ya mwanzo huyu ndiye Mungu muumbaji.
Kutoka 20:2-3 ‘‘Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miung mingine ila mimi. ”
MUHIMU: usitumie herufi ndogo mwanzoni unapo andika kumwakilisha Mungu wa muumbaji, ni kosa kubwa sana.
IBADA HUJUMUISHA YAFUATAYO; Kuadhimisha, kutoa sifa , kutoa sadaka ,kuomba na kumtumikia Mungu au mungu.
Ndipo akasimama Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zake makuhani , na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na ndugu zake, nao wakaijenga madhabahu ya Mungu wa Israel, ili kutoa sadaka za kuteketezwa juu yake, kama ilivyo andikwa katika toati ya Musa , mtu wa Mungu. Ezra 3:2
AINA ZA MADHABA
(i) Madhabahu ya Mungu wa mbinguni.
Je Baba yetu Ibrahimu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu.Yakobo 2:21.
Hii ni madhabahu ya kweli ambayo ndiyo iliyo sahii kwa mtu aliye mwamini Yesu kuijua kwa undani zaidi.
(ii) Madhabahu za kishetani. Paulo akasimama katikati ya Areopago, akasema, Enyi watu wa Athene , katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari mambo ya dini. Kwasababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona mambo ya Ibada yenu, naliona madhabahu iliyo andikwa maneno haya, KWA MUNGU ASIYE JULIKANA. Basi mimi nawahubiri habari zake yeye ambaye ninyi mnamwabudu bila kumjua. Matendo 17:22-23.
Ni dhahiri kwamba mtume paul aliyo iyona ni madhabahu ya kishetani ambayo ipo kinyume na mapenzi ya Mungu wa Kweli. Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.1korintho10:14-22. Ibada ya sanamu ni ipi? ni ibada inayo fanywa kwa mungu wa dunia hii, ambaye ni shetani.
HIZI NI BAADHI YA MADHABAHU ZA KISHETANI.
(a) Madhabahu za maji. Unaweza kuwa shahidi katika jambo hili yapo baadhi ya makabila ndani ya Nchi hii ya Tanzania na nchi nyingi duniani. Ambao hufanyia baadhi ya Ibada kwenye mito, baharini, maziwa na mabwawa katika maeneo haya watu huenda kutoa sadaka, au huita kutambika. Tambua maji yanasikia kwahiyo upo uhusiano mkubwa katika ulimwengu wa roho kati ya maneno yanayo tamkwa kipindi cha kutoa sadaka. Tusome 2wafalme 2:19-22 Watu wa mji wakamwambia Elisha, Angalia, twakusihi, mahali pa mji huu ni pazuri, kama Bwana wangu aonavyo; lakini maji yake hayafai, na nchi huzaa mapooza. Akaseme,Nileteeni chombo kipya, mtie chumvi ndani yake. Wakamletea. Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza. Hivyo yale maji yakapona hata leo, sawasawa na neno la Elisha alilolinena.
(b) Misitu na miti mikubwa. hii pia hutumika kama maeneo ya kufanyia Ibada za kishetani ambazo huusisha utoaji wa sadaka.
(c) Njia panda. Hili si geni kwa watu wengi katika miji na vijiji pia limekuwa likifanywa , kwa kutumia njia panda kama sehemu ya kutoa sadaka mbalimbali mfano; Nazi kuvunjwa, vibuyu kuvunjwa.
(d) Nguzo maalumu na minara. Haya yote yamekuwa maeneo ya kutolea sadaka katika miji mikubwa ambayo hasa vizazi na vizazi hulithi utamaduni huu.
(e) Milima. hasa milima mirefu hutumika kama maeneo muhimu katika Ibada za kishetani, na tambua kwamba tunapo ongelea ibada, Hakuna ibada pasipo kutoa sadaka. Swali ni kwamba sadaka hiyo inatolewa kwa nani ?
(f) Madhabahu za mateso.
Hizi humilikiwa na watu mfano, Wachawi, Waganga, Wanajimu na makuhani wa sanamu, hawa wote wanakuwa na kibali cha kipepo katika kuendesha ibada hizo ila kwa lengo la kutesa maisha ya watu tu.
Kazi yao ni kutengeneza Madhabahu hizo kwa ajili ya kupeleka Nguo, Majina, Picha,Vitu ,Fedha na visanamu vya watu wanaotaka wawatese. sababu hii hupelekea watumishi wa Mungu kuwafundisha sana, wakristo kuwa makini katika maisha yako ya kila siku ,una kula nini? Una vaa nini? Una ongea nini? yote haya katika ulimwengu wa roho yana umuhimu na yanaweza kumuonganisha mkristo hata yeye pasipo kujua.
Pamoja na kuangalia mfumo wa madhabahu za kishetani iko nguvu zaidi kwa madhabahu ya Mungu wa mbinguni. Mfano Elia na manabii. 1Wafalme 18:30-35, Jitahidi sana kuisoma habari hii yote na utaona jinsi ambavyo madhabahu ya ki-Mungu ilivyo na nguvu , ambazo ziliweza kumdhihirisha kuwa yeye ni Mungu mkuu.
MUHIMU: pasipo madhabahu hakuna msingi imara wa kiroho.
FAHAMU HATUA ZA KUJENGA MADHABAHU.
Jambo la kwanza fahamu ,Madhabahu zote za ki-Mungu lazima ziungamanishwe na kanisa lililopo hapa duniani.
Madhabahu yaweza kuwa ya mtu mmoja au kikundi cha watu wengi.
Mfano, Agano la kale Ezra 3:5 walitumia hasa kuchinja wanyama , ila kwa Agano jipya utaratibu hasa sa ni sadaka pasipo damu ya wanyama. Ila unaweza toa ; Pesa ,mnyama au kitu chochote
FAIDA YA MADHABAHU YA KI- MUNGU
(i) Huweka upatanisho (msingi)
Madhabahu ya ki-Mungu pale mwamini anapotoa sadaka, jambo la kwanza ni “UPATANISHO”
Mwanzo 18:6-10 ili Upatanisho uwe dhahiri ni endapo tu kutoa kutakuwa kwa moyo wa kupenda. Mfano unapo soma maandiko hayo yanaonyesha Baba wa Imani akifanya kwa kupenda na si kulazimiswa na watu, Ibrahimu alijua siri.
Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia , Ee Ibrahimu, Naye akasema , Mimi hapa. Akasema, umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye , Isaka , ukaende zako mpaka nchi ya moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu yam mlima mmojawapo nitakaokuambia. Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa. Mwanzo 22:1-3.
Kiukweli si kwamba Ibrahimu jambo hili katika hali ya kibinadamu lilikuwa lahisi kwake, ila mtumishi wa MUNGU huyu alijua maana ya madhabahu, Madhabahu unapo jenga huanzia rohoni kwanza kwahiyo pale alipo kubali kumtoa Isaka Kuwa sadaka ya kuteketezwa tayari alikuwa amejenga.
MUHIMU: Kwa kila jimbo, ulifanyalo kuwa makini katika kujenga Madhabahu.
(ii) Hufungulia Baraka.
Kupitia Madhabahu ya Mungu wa Israel, inaleta baraka za haki isivyo kawaida.
Ukisoma, Mwanzo 22:15-18 ''Malaika wa BWANA akamwita Ibrahimu mara ya pili kutoka mbinguni. akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.''
Katika maisha yako ya kawaida jitahidi kabla ya kuomba Baraka, fanya kitu kwanza mbele za Mungu.
Soma maneno haya pia utaona jinsi Mungu anavyo toa maagizo kwa balaamu kuwa akanene na Baraki.Hesabu 23:16-20
Jitahidi upitie vifungu hivi pia vitakavyo kujenga sana juu ya baraka za KiMungu.
''na Baraka hizi zote zitakujulia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako. Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani'' Kumb 28; 2, 8.
''Atawabarikia wamchao BWANA, Wadogo kwa wa kubwa.'' zaburi 115:13
Atukuzwe Mungu , Baba wa Bwana wetu Yesu kristo, aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni , katika ulimwengu wa roho, ndani yake kristo. Efe 1:3
MUHIMU: tambua mambo ya rohoni huzaa na baadaye huja ya kimwili. Galatia 3:9 Unapofanya jambo hili Imani huitajika sana.
Tulio mwamini Yesu, wote tumebarikiwa ili kuzifanya Baraka ziwe dhahiri maishani mwako LAZIMA UFANYE KITU. Matendo ya mitume 3:25-26. ''Ninyi mmekuwa watoto wa Manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na Baba zenu, akimwambia Ibrahimu, katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa.''
(iii) Ulinzi wa Ki-Mungu.

Tambua Mungu wetu ni Mungu wa Maagano huachilia ulinzi katika maisha ya mtu kwasababu pale anapo mtazama mtu huyo huona “AGANO”. Mfano, ukisoma mandiko haya yote yanazidi kuonyesha faida ya maagano. Nuhu, Mwanzo 6:18, 9:11. ''Lakini nitafanya agano langu nawe kuwa thabiti; nawe utaingia katika safina, wewe na wanao, na mkeo na wake za wanao, pamoja nawe. na agano langu nitalithibitisha nanyi, wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya gharika; wala hakutakuwa tena gharika , baada ya hayo, kuiharibu nchi.''
Maandiko yote haya yanaonyesha kuwa kupitia sadaka huweka agano ambalo Mungu huliangalia hilo kwa kipindi kirefu sana.
Ibrahimu, Mwanzo 17:4 ''mimi, agano langu nimefanya nawe, nawe utakuwa baba wa mataifa mengi.'' Mungu wetu ni Mungu wa Maagano yeye huweka na hilo agano hudumu kwa kipindi kirefu sana, unapo toa sadaka inakuwa agano mbele za Mungu ambalo hudumu kwa kipindi kirefu sana.
Kumb 29:25 ‘‘Ndipo watakaposema watu, ni kwa kuwa waliacha agano la BWANA, Mungu wa baba zao, alilofanya nao hapo alipowatoa katika nchi ya Misri’’.
(iv) Humkumbusha Mungu. Jambo hili ni siri kubwa sana, Madhabahu huongea yaani Inasema mbele za Mungu. Zaburi 106:45 ''Akawakumbukia agano lake ; Akawahurumia kwa wingi wa fadhiri zake.''
Ufunuo 16:7a.''Nikasikia hiyo madhabah ikisema'' Kwahiyo katika maisha ukiwa kama mwamini unapo kuwa na tabia ya kujenga madhabahu kwa mambo uyafanyayo ,kwasababu kutokana na shughuri mbalimbali za kimaisha upo wakati utasahau wewe binafsi kama ulifanya kitu mbele za Mungu, ila Hiyo Madhabahu “ITASEMA MBELE ZA MUNGU KWAAJILI YAKO”
(V) Humdhiirisha Mungu au humfunua. 1wafalme 18:22, 32-38 ukisoma vizuri na kwa umakini utagundua kuwa ugomvi au ubishani uliokuwepo kati ya nabii Eliya na Manabii wa Baali ulikuwa nani Mungu wa kweli kati ya Mungu wa Eliya na wao Baali, ubishano wao ulikuwa mkubwa sana ambao usingwezwa kuisha kwa uhalaka kwasababu IMANI ni kitu cha thamani kwa mtu aliye nacho ,pale anapo amini juu ya jambo fulani si kwa ulahisi unaweza mwambia usiamini, ni mpaka pale UDHIHIRISHO unapo tokea. Kwahiyo Nabii Eliya akawaambia ‘‘kwa hiyo na watutolee ng’ombe wawili; wao na wajichagulie ng’ombe mmoja, wamkate-kate na kumweka juu ya kuni, wasitie moto chini; nami nitamtengeza ng’ombe wa pili, na kumweka juu ya kuni,wala sitatia moto chini. Nanyi ombeni kwa jina la mungu wenu, nami nitaomba kwa jina la bwana; na Mungu yule ajibuye kwa moto, na awe ndiye Mungu”.
Kiukweli katika maneno hayo, kinacho tamkwa ni kwamba LEO NA TUONE NANI ALIYE WA KWELI KATI YA mungu au MUNGU.
KITU CHA KUFANYA
Kama hukuwahi kujenga madhabahu jitahidi kujitoa kwanza kwa kujengea vitu vyako vyote ukianzia ,watoto wako, ndugu kiujumla. elimu ,biashara ili uviungamanishe na Mungu, pia baada ya kuyajua yote haya ,JITAHIDI UYAFANYIE KAZI NA MUNGU WA MBINGUNI AKUBARIKI.

Wednesday, 6 September 2017

KUBENEANA MIZIGO

.                       *KUBEBEANA MIZIGO*

*_”Nikamwelekezea Bwana Mungu uso wangu, ili kutaka kwa maombi, na dua, pamoja na kufunga, na kuvaa nguo za magunia na majivu. Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri Zake.”_ (Danieli 9:3, 4).*

Akiwa na mzigo kwa niaba ya Israeli, Danieli alijifunza upya unabii wa Yeremia. Ulikuwa waziwazi kiasi ambacho kwenye vitabu alielewa shuhuda hizi zilizorekodiwa “hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.”

Kwa imani ambayo msingi wake ulikuwa kwenye neno la unabii lililo imara zaidi, Danieli alimsihi Bwana kwa ajili ya kutimizwa upesi kwa unabii huu. Alisihi kwa ajili ya heshima ya Mungu kudumishwa. Katika ombi lake alijiweka yeye mwenyewe kikamilifu pamoja na wale waliokuwa wamepungua katika makusudi ya Mungu, akiungama dhambi zao kana kwamba ni zake mwenyewe.

Ombi lililotoka kwenye midomo ya Danieli lilikuwa la ajabu sana! Linadhihirisha nafsi iliyonyenyekea kiasi cha ajabu! Joto la moto wa kimbingu lilitambulika katika maneno yaliyokuwa yakipanda juu kwa Mungu. Mbingu ilijibu ombi lile kwa kumtuma mjumbe wake kwa Danieli. Katika siku zetu hizi, sala zinazowasilishwa namna hiyo zitashinda pamoja na Mungu. “Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana.”

Kama ilivyokuwa nyakati za kale, ombi lilipotolewa, moto ulishuka kutoka mbinguni na kuteketeza kafara iliyokuwa juu ya madhabahu; hivyo, kama majibu kwa ajili ya maombi yetu, moto wa kimbingu utakuja kwenye roho zetu. Nuru na uwezo wa Roho Mtakatifu vitakuwa vyetu. Je, sisi hatuna hitaji kubwa la kumwita Mungu kama alivyokuwa Danieli? Ninanena na wale wanaoamini kwamba tunaishi kwenye kipindi cha mwisho kabisa cha historia ya dunia hii. Ninawasihi mbebe mioyoni mwenu mzigo kwa ajili ya makanisa yetu, shule zetu na taasisi zetu.

Mungu yule aliyesikia maombi ya Danieli atasikia maombi yetu tunapomjia kwa moyo wa toba. Mahitaji yetu ni ya muhimu pia, matatizo yetu ni makubwa na tunahitaji kuwa na makusudi yenye mkazo uleule, na kwa imani tumtwike mzigo wetu yeye aliye Mbeba-mizigo mkuu. Lipo hitaji kwa ajili ya mioyo kuguswa sana wakati wetu kama ilivyokuwa wakati Danieli alipoomba.

Tuesday, 5 September 2017

UONGOZI WA MUNGU ALIOKUSUDIA HAUFANANI NA MATARAJIO YETU

Uongozi wa Mungu aliokusudia haufanani na makusudio yetu.

1 Nyakati 28:3 Lakini Mungu akaniambia, wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu,kwa sababu umekuwa mtu wa vita,nawe umemwaga damu.

1.Kuna viongozi ambao ni wazuri sana katika vita lakini kuna maeneo ambayo hawafai kabisa kuwa viongozi bali ni maeneo yanayohusika na Vita tu!!. Ni kosa kubwa kumpa sehemu ambayo sio ya Vita aongoze.

2.Haya ni mambo ambayo Mungu aliyaona kwa Daudi mtumishi wake aliyemchagua yeye mwenyewe na alikataa asijenge hekalu au sehemu ya kuabudia. Sio kwamba hakuwa kiongozi mzuri bali uongozi huo uliohusika kwenye hilo eneo hakustahili kabisa .

3.Haya ni makosa ambayo tumekuwa tunayafanya maeneo mbalimbali tukiona mtu amefanya vizuri eneo moja tunamkabidhi maeneo yote bila kujua mikono yake ni ya Vita au ya uongozi wa kawaida.Haya mambo yametokea katika mataifa mengi waliopigania uhuru walijiweka kwenye ngazi za juu za uongozi au waliookoa baadhi ya nchi kwenye majanga na vita. Asilimia kubwa ya hawa mikono yao sio salama kwa raia na wapinzani wao. Ndo maana hata watu wakiumia au kupata majanga kwao haiwasumbui. Maana wao ni viongozi wa vita Na sio wa kawaida.

4.Haya ni mambo ambayo yamekuwa yanaleta shida hata makanisani na nyumba za ibada. Mtu akiombea mtu mguu ukapona tunamshauri awe Mchungaji wakati hana hata chembe moja ya kuwa mchungaji au kiongozi wa ibada. Ndo maana tuna viongozi wengi hawana neno wala hekima lakini wana kigezo cha miujiza na uponyaji.

5.Kuna watu ambao hawafai kupewa kila uongozi maana madhara yake ni makubwa maana kuna eneo ambalo linahitaji hekima huruma na uangalifu mkubwa ndo maana Mungu amegawa nafasi kwa kila kabila na kazi zake japo zinaweza kuingiliana kwa hekima yake.

6.Ni vigumu sana kumweka mfugaji awe mfanyabiashara maana Mungu alichoweka ndani yake ni ufugaji,kosa ni pale utakapompa biashara ataiendesha kifugaji na baada ya muda itakufa maana mikono Yake ni ya mifugo.

7.Kuna watu wenye roho za kivita na mikono ya kivita hawa usitegemee watakuwa na huruma (sio wabaya kabisa) Ila hawafai kwa kila kazi.Hii ndo nafasi ambayo Mungu aliiona na kuizuia kwa Daudi.

8 Kuna mikono yenye baraka kwa kazi mbalimbali ndo maana unasikia flani ana mkono WA ufugaji, kilimo,biashara,udaktari na mambo mengine.

9.Jifunze kuomba Mungu akupe kiongozi sahihi na eneo sahihi linalompasa kuongoza.

10.Usimwamini kiongozi kuliko Mungu ili upate nafasi ya kuona madhaifu yake na kumpeleka kwenye nafasi husika kwa kutumia maombi.

11.Omba Mungu atupe kukaa kila mtu kwenye nafasi yake na kwa muda unaotakiwa.

12.Omba uongozi wa aina zote utanguliwe na Mungu na nafasi zote ziheshimu ukuu wa Mungu na kuheshimu nafasi nyingine.

Mungu akubariki

FAHARI YA KIJANA NI NGUVU ZAKO

Bwana Yesu Kristo atukuzwe wana wa Mungu aliye hai.
Ninazidi kumshuru Mungu kwa ulinzi wake na kuzidi kutukutanisha tena, jina la Bwana lihimidiwe.

Karibu sana mpendwa tusemezane katika ujumbe huu wa neno la Mungu ambao Roho wa Mungu ametupatia.

Ujumbe:FAHARI YA KIJANA NI NGUVU ZAKO.
               ======================

Katiika ujumbe wetu naomba kuzungumza na kusemezana na vijana wote wa kike na wa kiume,na labda Roho wa Mungu atasema nawe hata kama sio kijana basi naomba ulipokee neno hilo litakusaidia.

         Tusome MITHALI 20:29

Fahari ya kijana ni nguvu zao;Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.

Nguvu
---------- Ni uwezo unaomsababisha mtu kufanya jambo Fulani katika maisha yake.

➡Hizo nguvu ambazo unazo wewe kijana,naomba nikuambie kwamba Mungu hajakupa nguvu hizo kwa ajili ya:
👉Kuiba,kubaka,kubomoa nyumba za watu,wala hujapewa nguvu hizo kwa ajili ya kupiga watu,wala sio za kutukana wazee mitaani.

👉Bali  Mungu amekupa nguvu hizo kwa ajili ya kumtumikia,kwa ajili ya kufanya kazi nzuri za mikono yako naye akubariki,kwa ajili ya kuwasaidia wengine mpendwa.
➡Hivyo Tumia nguvu ulizonazo leo kumtumikia Mungu wako kijana wangu.

👉Lakini vijana wengi Leo tunazitumia hizo nguvu zetu vibaya sana nakuambia mpendwa; wengine wanazitumia kuvuta madawa ya kulevya,wengine kuiba,wengine kubaka mitaani,wengine kupigana,wengine kutukana watu.

➡Nakuambia wewe kijana utumiaye nguvu zako vibaya wakati wa ujana wako,nakuambia siku inakuja ambayo utazitafuta nguvu hizo.
➡Wengine husema siwezi kumtumikia Mungu nikiwa kijana,Bali nitamtumikia Mungu nikiwa mzee,hivi calender ya maisha yako unayo wewe mikononi mwako?.

      Soma hii hapa MHUBIRI 12:1-2

1⃣Mkumbuke muumba wako siku za ujana wako,Kabla hazijaja siku zilizo mbaya,Wala haijakaribia miaka utakaposema,Mimi sina furaha katika hiyo.

2⃣Kabla jua,Na nuru na mwezi,na Nyota havijatiwa Giza;Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;....

👉Unaona hapo 👆wewe kijana mwenzangu;neno linakuambia tumkumbuke Muumba wetu ambaye ni Mungu wetu katika siku za ujana wetu,kumbuka  kumtumikia BWANA Eee kijana .
➡Nakushangaa wewe unayesema kwamba unasubiri uwe mzee ndio utamtumikia Mungu.

👉Siku zinakuja wewe kijana ambazo hizo nguvu zako unazoziaribu Leo utazitafuta nakuambia.
➡Mungu anataka tumtumikie Maishani mwetu tukiwa bado tuna nguvu wapendwa.
➡Usisubiri umekuwa mgonjwa ndio sasa unakumbuka Mungu yupo,jitambue bado usiku haujakufikia mpendwa.

👉Acha kutumia nguvu zako kuwatukana wazee nakuambia kijana mwenzangu.Wewe ujajivunia huo ujana wako na kuanza kuwadharua na kuwatukana wazee,nakuambia huyo mzee unayemtukana na kumdharau alikuwa kijana kama wewe.

👉Yaani kinywa chako kimejaa matusi,maneno machafu dhidi ya wazee,nakuambia ole kwako.
➡Unajivunia nguvu zako kwa kuvuta bangi,naomba nikuambie kwamba hata na huyo mzee nguvu alikuwa nazo.

Wahenga walisema kwamba:
➡Kuishi kwingi ni kuona mengi√.
Sasa wewe huyo mzee unayemdharau alishayaona mengi sana,je utaomba ushauri kwake? Muheshimu mzee mpendwa kijana.

➡Tambua kwamba Wewe sio wa kwanza kuwa kijana,wapo waliokutangulia wewe ambao waliwaheshimu wazee wao na maisha yao yakawa mazuri sana,na Mungu akawafanikisha na kuwainua zaidi.

      Ona vijana hawa:

👉Kijana Yoshua alimuheshimu sana Musa,na baada ya kifo cha Musa Mungu akamuinua Yeye.

👉Kijana Samweli alimuheshimu sana Eli na akawa kijiana mwenye maadili mema,na Mungu akamtumia zaidi.

👉Kijana Timotheo alimuheshimu Paulo.
Na wengine wengi mpendwa ambao waliwaheshimu wazee wao;waliyasikiliza mausi,ushauri na maonyo yao, na Mungu akawainua zaidi na zaidi;kwanini wewe unamdharau mzee huyo?

👉Ni kweli kwamba Mungu ameiweka huduma kubwa ndani yako,lakini tambua unahitaji ushauri wa wazee ili uzidi kusonga mbele zaidi;acha kuwadharau na kuwatukana ewe kijana mwenzangu.

Jambo la kusikitisha ni kwamba:

➡Vijana wengi makanisani wakiinuliwa kihuduma,basi wanasema yatosha.

~Wakisomea Biblia na kupata diploma, degree, masters ya teologia basi wanajiona kwamba wamemaliza yote.

👉Wakijuwa kuimba,kupiga guitar basi wanasema yatosha.Wala hawapendi kuomba ushauri kwa wazee,mzee akimshauri utasikia wewe mzee wakati wako umekwisha,tuachie vijana.
➡Ni kweli wakati wake umekwishapita lakini sikiliza ushauri,Maonyo yake akuambiayo.
Ewe kijana nakushauri kwa huruma zake Mungu acha kumdharau mzee,Bali muheshimu sana maana huyo ni adhina kubwa kwako mpendwa.

             1TIMOTHEO 4:11-12.

👉Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha.

👉Mtu awayeyote asidharau ujana wako,Bali uwe kielelezo kwao waaminio,katika usemi na mwenendo,na katika upendo na imani na usafi.

➡Lakini vijana wengi tunadharaulisha ujana wetu kwa matendo yetu mabaya katika jamii,ndimi zetu zimejaa matusi tuuuu,hivi kwa mwenendo wako huo utakuwaje kielelezo kwa watu? Jirekebishe kijana mwenye tabia mbovu na mbaya,la sivyo utaeendelea kuudharaisha ujana wako,na imani yako inakuwa sio kitu.

➡Acha kuudharaulisha ujana wako wewe kijana mwenzangu.
Na wewe mzee wangu kichwa chako kinathamani kubwa sana endapo kitaonekana katika njia bora ambayo inampendeza Mungu, usiwe wewe mwenyewe ndio chanzo cha kujidharaulisha mbele ya vijana,vijana tunahitaji maonyo yako,tunahitaji ushauri wako ili tusonge mbele zaidi,hivyo thamanisha uzee wako lakini pia thaminisha kichwa chako chenye mvi.Wewe ni adhina kubwa kwetu sisi vijana,jitambue nakuambia.

👉Vijana wenzangu naomba niwashauri kwamba Tusiwaige wale vijana waliomdhiaki Mtumishi wa Mungu Elisha,hatimaye wakaliwa na Dubu;Bali tuwaige wale vijana waliomuinua Musa mikono yake; Tuishi pamoja na wazee wetu,tutachota mambo makubwa kutoka kwao.

➡Ushirika wetu na wazee nakuambia utakufanya uonekane kuwa ni kijana unayeifahaa jamaa ya waaminio na hata wasioamini pia,kwa mwenendo wako safi nakuambia utawavuta wengine kuja kwa Yesu Kristo ya kuziokoa nafsi zao na mauti.
~Tukae bega kwa Bega na wazee wetu Mungu atatufanikisha na kutuinua zaidi wapendwa.

➡Tusiwadharau wazee,tuwaheshimu sana,tuombe ushauri kwa wazee ndugu zangu Mungu atatufanikisha.
➡Tumia nguvu zako vema mpendwa maana nguvu zako ndio fahari yako.

👉Thamani ya ujana wako iko mikononi mwako,thamani ya UJANA wako ni nguvu zako, Tumia Nguvu zako vizuri.
➡Usitarajie kuheshimiwa kama wewe mwenyewe hujajiheshimu mpendwa.
➡Thaminisha,Heshimisha ujana wako ewe kijana mwenzangu.

👉Kijana Mungu anahitaji umtumikie siku za ujana wako mpendwa, kabla hazijaja siku mbaya kwako.
➡Chunguza Sana ujana  wako leo.
➡Unaandikiwa  wewe kijana Maana unazo nguvu, na NENO la BWANA linakaa ndani yako. Nawe utamshinda huyu shetani kwa nguvu za NENO La Mungu ndani yako.

👉Kijana Jaza NENO la Mungu moyoni mwako nalo NENO litakuongoza Katika njia ikupasayo.

Monday, 4 September 2017

TAFUTA AMANI NA WATU WOTE

Shalom KANISA

TAFUTA AMANI NA MUNGU
Mithali 8:17 "
Nawapenda wale wanipendao, Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona. "
Isaiah 55:6
Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;
Waebrania 12:14
Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Yohana 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
UNAPENDWA NA MUNGU!
Wewe ni wa thamani sana hata kama haujui! Mungu anakupenda! Alimtoa kristo akafa msalabani ili kulipa deni la dhambi zetu zote tulizofanya na kumwasi mungu kwani.Thamani ya ko ni Damu ya Mwana wa Mungu isiyo na ila wala dhambi...Halleluyah,Unapendwa!
1Peter 1:18-19 "18
"Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
20 Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu; 21 ambao kwa yeye mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu."
Umeamini? Unapendwa! Kristo alikuwepo miaka mingi mingi milele yote,lakini alifunuliwa kwajili yetu sote,mimi na wewe, sisi ni sababu hasa ya kristo kuja ulimwenguni. Unapendwa!
UNAMHITAJI YESU KRISTO,FANYA UAMUZI SASA UMKARIBISHE MAISHANI MWAKO.
Hizi ndio sababu kwa nini unamhitaji Yesu kristo:
Warumi 3:23 " kwa sababu wote wamefanya dhamb i, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;"
Warumi 5:12 Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;
Maandiko yanaendelea kueleza juu ya huyu Yesu kristo inasema katika
"Warumi 5:18-19
18 Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki watu wote walihesabiwa haki yenye uzima. 19 Kwa sababu kama kwa kuasi kwake mtu mmoja watu wengi waliingizwa katika hali ya wenye dhambi, kadhalika kwa kutii kwake mmoja watu wengi wameingizwa katika hali ya wenye haki."
UNATAKIWA KUFANYA NINI?
Hebu tuone hapa jinsi maandiko yanavyotupa jibu:
Matendo ya mitume 2:37-40
"Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.39 Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.40 Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.
Matendo ya Mitume 16:30-31
" kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka?Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako."
Inawezekana nawe unajiuliza ya kwamba unawezaje kupokea kipawa hiki cha Mungu cha wokovu kwa njia ya Yesu Kristo ukisema na kuuliza moyoni
"Tutendeje, ndugu zetu?".Jibu linapatikana unatakiwa kufanya yafuatayo:
1.Tubu dhambi zako zote ulizotenda mbele ya Mungu kwa kumwambia kwamba umekosa na muombe akusamehe na akupe nguvu ya kushinda hiyo dhambi ili usije ukaanguka tena.atakusamehe na kukupokea ikiwa utafanya hivyo kwa moyo wako wote na kwa imani. Pia
"Mithali 28:13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema."
2.Mwamini Bwana Yesu na mkaribishe kwenye moyo wako na maisha yako. Ni Yesu pekee ndio mwokozi wa ulimwengu na hakuna njia nyingine yoyote ile ya kumfikia Mungu isipokuwa kristo Yesu hata anasema mwenyewe
"Yohana 14:6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. "
3.Liitie Jina la Yesu
Tunaokolewa kwa kupitia jina moja tu! vizazi vyote na jamii yote ya mwanadamu tunaokolewa kwa jina la yesu. JINA LA YESU NDILO LILILOBEBA WOKOVU WA KILA MWANADAMU
Imesemwa katika Mathayo 1:21 "Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao." pia anasema
Matendo ya Mitume 2:21 "Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa."
Warumi 10:13 " kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka."
Usiache nafasi hii ikupite bila ya kuliitia jina la Yesu hakika litafanya kazi kwako!
Liitie Jina la YESU KRISTO kwanjia ya maombi toka moyoni mwako na mwombe Bwana akusamehe dhambi zako zote nawe utaokoka sasa! hivyohivyo ulivyo Kristo anakupenda na kamwe hatakutupa ukimwendea.kwa ahadi hii hakikisha umefanya uamuzi wa kumpa kristo maisha yako .
Yohana 6:37
"Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe."
Yohana 6:35
"Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe."
Biblia katika Yohana 12:44-50 inasema:
"Naye Yesu akapaza sauti, akasema,
Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi bali yeye aliyenipeleka.45 Naye anitazamaye mimi amtazama yeye aliyenipeleka.
46 Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani. 47 Na mtu akiyasikia maneno yangu, asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.
48 Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho. 49 Kwa sababu mimi sikunena kwa nafsi yangu tu; bali Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.
50 Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi, kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo.
Je nawewe ni miongoni ambao bado unamkataa YESU na maneno yake? lini utamkubali na kumwamini?.kumbuka YESU Ni MWOKOZI WAKO,AMEKUFIA MSALABANI na saa ya wokovu ni sasa FANYA MAAMUZI YA KUMFUATA KRISTO!.
Sali sala hii fupi toka moyoniUkimtazama na kuamini kwamba Mungu anakusikia kama umeamua kumwamini yesu na unataka atawale maishani mwako,akupe furaha amani na msamaha wa dhambi na akufanye kuwa mwana wa mungu sawasawa na alivyoahidi omba ukisema:
"BWANA YESU NINAKUJA KWAKO MIMI NI MWENYE DHAMBI NINAOMBA UNISAMEHE NA KUNIOKOA.KARIBU KWENYE MAISHA YANGU NA MOYO WANGU,UNISAMEHE MAOVU YANGU YOTE,UNIOSHE NA KUNITAKASA.KUANZIA SASA MIMI NI WAKO.NINAKUSHUKURU KWA KUWA ULIKUFA MSALABANI KWA AJILI YA DHAMBI ZANGU NA KWA KUNIPOKEA.SASA NIMEOKOKA.MIMI NI MWANA WA MUNGU,
Amen"
Sasa ndo umeokoka ivyo, Kristo ameingia ndani yako,wewe sasa umekuwa kiumbe kipya kwani anasema katika
"2Wakorintho 5:17
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya ; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. " pia ahadi hii inakuhusu sana anasema "
Yohana 1:12
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; "
Mambo ya kuzingatia:
1. Zungumza na Mungu kwa maombi kila siku (Yohana 15:7)
2. Soma Neno la Mungu (Biblia) kila siku (Matendo ya Mitume 17:11)
3. Mruhusu Roho Mtakatifu akutawale (Wagalatia 5:16-25; Warumi 8:14-17)
4. Umtumaini Mungu kwa kila jambo katika maisha yako (1Petro 5:7; Zekaria 4:6)
5. Usiache kukusanyika na kushirikiana na wengine waliompokea Yesu Kristo kuwa Mwokozi wao kama wewe ili uimarike zaidi (Waebrania 10:25)
Unapendwa!
MUNGU wa mbinguni ni Baba yako.sema naye kwanjia ya maombi na sikia kutoka kwake kwanjia ya kusoma Biblia.Kama unapata shida.
Jenga mazoea ya Kusoma Biblia nakushauri anza na kitabu cha Yohana Mtakatifu,ukimaliza Soma Warumi halafu malizia Biblia yote katika hali ya maombi na kumwamini Mungu utashangaa kuona jinsi Mungu anavyokupenda na alivyo kuahidia mambo mazuri mno katika ulimwengu wa sasa na ule unaokuja baada ya kufa.Omba usiache.

MADHABAHU

MADHABAHU ni mahali rasmi ambapo watu au mtu hutumia kufanya ibada kwa Mungu au mungu ambaye ndiye mwabudiwa. Kuna utofauti kati ya mungu wa...