Tuesday, 5 September 2017

UONGOZI WA MUNGU ALIOKUSUDIA HAUFANANI NA MATARAJIO YETU

Uongozi wa Mungu aliokusudia haufanani na makusudio yetu.

1 Nyakati 28:3 Lakini Mungu akaniambia, wewe hutajenga nyumba kwa ajili ya jina langu,kwa sababu umekuwa mtu wa vita,nawe umemwaga damu.

1.Kuna viongozi ambao ni wazuri sana katika vita lakini kuna maeneo ambayo hawafai kabisa kuwa viongozi bali ni maeneo yanayohusika na Vita tu!!. Ni kosa kubwa kumpa sehemu ambayo sio ya Vita aongoze.

2.Haya ni mambo ambayo Mungu aliyaona kwa Daudi mtumishi wake aliyemchagua yeye mwenyewe na alikataa asijenge hekalu au sehemu ya kuabudia. Sio kwamba hakuwa kiongozi mzuri bali uongozi huo uliohusika kwenye hilo eneo hakustahili kabisa .

3.Haya ni makosa ambayo tumekuwa tunayafanya maeneo mbalimbali tukiona mtu amefanya vizuri eneo moja tunamkabidhi maeneo yote bila kujua mikono yake ni ya Vita au ya uongozi wa kawaida.Haya mambo yametokea katika mataifa mengi waliopigania uhuru walijiweka kwenye ngazi za juu za uongozi au waliookoa baadhi ya nchi kwenye majanga na vita. Asilimia kubwa ya hawa mikono yao sio salama kwa raia na wapinzani wao. Ndo maana hata watu wakiumia au kupata majanga kwao haiwasumbui. Maana wao ni viongozi wa vita Na sio wa kawaida.

4.Haya ni mambo ambayo yamekuwa yanaleta shida hata makanisani na nyumba za ibada. Mtu akiombea mtu mguu ukapona tunamshauri awe Mchungaji wakati hana hata chembe moja ya kuwa mchungaji au kiongozi wa ibada. Ndo maana tuna viongozi wengi hawana neno wala hekima lakini wana kigezo cha miujiza na uponyaji.

5.Kuna watu ambao hawafai kupewa kila uongozi maana madhara yake ni makubwa maana kuna eneo ambalo linahitaji hekima huruma na uangalifu mkubwa ndo maana Mungu amegawa nafasi kwa kila kabila na kazi zake japo zinaweza kuingiliana kwa hekima yake.

6.Ni vigumu sana kumweka mfugaji awe mfanyabiashara maana Mungu alichoweka ndani yake ni ufugaji,kosa ni pale utakapompa biashara ataiendesha kifugaji na baada ya muda itakufa maana mikono Yake ni ya mifugo.

7.Kuna watu wenye roho za kivita na mikono ya kivita hawa usitegemee watakuwa na huruma (sio wabaya kabisa) Ila hawafai kwa kila kazi.Hii ndo nafasi ambayo Mungu aliiona na kuizuia kwa Daudi.

8 Kuna mikono yenye baraka kwa kazi mbalimbali ndo maana unasikia flani ana mkono WA ufugaji, kilimo,biashara,udaktari na mambo mengine.

9.Jifunze kuomba Mungu akupe kiongozi sahihi na eneo sahihi linalompasa kuongoza.

10.Usimwamini kiongozi kuliko Mungu ili upate nafasi ya kuona madhaifu yake na kumpeleka kwenye nafasi husika kwa kutumia maombi.

11.Omba Mungu atupe kukaa kila mtu kwenye nafasi yake na kwa muda unaotakiwa.

12.Omba uongozi wa aina zote utanguliwe na Mungu na nafasi zote ziheshimu ukuu wa Mungu na kuheshimu nafasi nyingine.

Mungu akubariki

No comments:

Post a Comment

MADHABAHU

MADHABAHU ni mahali rasmi ambapo watu au mtu hutumia kufanya ibada kwa Mungu au mungu ambaye ndiye mwabudiwa. Kuna utofauti kati ya mungu wa...